Before You Call Yourself A Founder, There’s Something You Need To Understand
The hard truth ni hii: building a startup in Kenya si mchezo. Una-build product while bado unaeducate market juu wengi hawajaelewa problem unajaribu solve. Una-compete na established companies zenye ziko na teams kubwa, marketing budget kubwa, na customer trust yenye wewe bado unatafuta. Sometimes unapata great idea but funding hakuna. Sometimes customers wanasema wanapenda solution yako lakini hawako ready kulipia. Na worse, unaweza spend months building something then market ikushow brutally ati demand haiko venye ulidhania. Hiyo rejection cycle ndio founders wengi hupitia quietly bila kusema.
Lakini challenge biggest si competition. Challenge biggest ni psychological pressure. Imagine kuamka kila siku ukijua watu wengine wanangoja salary mwisho wa mwezi while wewe hujui next three months zitakaa aje. Friends wako wanaendelea na stable careers, wengine wanaonekana progressing fast, alafu wewe uko hapo ukibet years za life yako kwa idea yenye hakuna guarantee ita-work. Hapo ndio entrepreneurship hukutest beyond business. Inatest patience, discipline, confidence na ability ya kusurvive uncertainty bila kupoteza focus.
Na bado despite hiyo pressure yote, startup founders wanaendelea kujenga. Why? Ju every major company tunaona leo ilianza kama risky idea mahali fulani. Truth ni hii: entrepreneurship Kenya si Roses kama vile social media huipaint. Ni mchezo wa resilience. Mara mingi si the smartest founder hushinda. Ni yule ana-survive long enough mpaka apate breakthrough. So kama uko kwa startup journey na unafeel pressure, understand that you are not only building business Pia Una-build capacity ya kufanya vitu wengi hawawezi endure.
Question ni hii: uko ready kuvumilia reality ya entrepreneurship… ama ulipenda tu idea ya kuitwa founder?


Comments
Post a Comment