Skip to main content

School Taught Us How To Work… But Nobody Taught Us These Money Rules

 




Wasee wengi huku Kenya wamegrow wakiamini formula moja rahisi sana: soma vizuri, pata job, fanya kazi hard, save pesa… maisha itajipa eventually. Lakini reality ya world ya leo imechange vibaya sana. Cost of living inapanda kila mwaka, opportunities zinabadilika faster, na kufanya kazi hard peke yake haiguarantee financial freedom kama venye watu walikuwa wanaamini before. 


Truth ni hii watu wengi wanachase pesa, but very few wanajifunza rules za pesa. Na hapo ndio tofauti huanza kujitokeza kati ya watu wanaendelea kujenga wealth quietly na wale wanaendelea kuhustle mwaka hadi mwaka lakini financial position yao haichange sana.


Kuna principle moja wealthy people wanaelewa mapema sana: money lazima ikuwe employee wako, si wewe kuwa employee wa pesa forever. Hii ndio reason investment knowledge ni muhimu kuliko venye watu wengi wanafikiria. Ukiishi maisha ya kutumia kila kitu unaearn, without building assets zenye zinaweza kukugeneratea income in the future, unaeza kufanya kazi miaka 30 lakini bado ukue dependent on active income daily. 


Financial freedom haikuji juu unaearn more pekee yake inakuja juu unaelewa design ya kufanya pesa yako ikuwe system yenye inaendelea kukugrow hata ukiwa offline.


Na ndio maana kuna certain investment rules kila mtu anafaa kuelewa mapema. Rule kama kujua tofauti ya asset na liability. Rule ya kuelewa compound growth na venye small consistent investments hugeuka big money after years. Rule ya kutoweka pesa yote mahali moja juu risk ikikugonga unaanza from zero. Rule ya kujua ati lifestyle inflation inaweza kufanya salary yako ikiongezeka lakini wealth yako ibaki same. Most people huanza kufikiria hizi vitu too late after years mingi ya kufanya kazi lakini hakuna solid financial progress ya kuonyesha.


The dangerous thing ni ati society imetufunza how to earn money… but rarely hutufunza how to make money stay, grow, and multiply. Ndiyo maana unaweza pata mtu anaearn vizuri lakini bado ako financially stressed kuliko mtu mwingine anaearn kidogo but understands investing better. Difference si effort pekee. Difference ni financial knowledge.


Question ya ukweli ni hii: 


unaendelea kufanya kazi for money everyday… ama kuna system una-build yenye siku moja pesa itaanza kufanya kazi for you? Ju mwisho wa siku, freedom ya kweli haikuji juu ulihustle harder kuliko wengine. Mara nyingi huja juu ulijifunza rules ambazo wengi walignore mapema.


]

Book Recommendation



Comments

Popular posts from this blog

Hii Ndio Reason why Unafaa Uchukulie Hustle yako very Serious...

Kuna story iliuma wasee wengi sana kutoka Kisii County back in 2021. Villagers kadhaa walichomwa na moto baada ya kushukiwa kushukiwa ya kwamba ni wachawi.  Ukiangalia juu juu unaweza sema hii ni story ya superstition ama mob justice. Lakini ukiingia ndani zaidi, unaona reality yenye huwa painful sana kwa society nyingi za Africa: mara nyingi mnyonge hana haki . Watu ambao hawana nguvu, hawana pesa, hawana influence, wakipatikana kwa mazingira ya accusation, mara nyingi hawana sauti ya kujitetea. Na history imetuonyesha kitu moja consistently: poverty inafanya mtu akuwe vulnerable sana kwa systems, kwa jamii na hata kwa injustice ya watu wengine. Na ndio maana hii generation yetu inafaa kuchukulia economic empowerment serious kuliko venye tunafanya saa hii. Ukianza biashara, ukijenga skills, ukisaka financial freedom, remember that hii si story ya wewe tu kununua gari ama kuishi maisha soft. Ni story inahusu kuhakikisha watoto wako, familia yako na generation yako hawafiki place ...

A Complete Guide for Turnover Tax for Small Businesses in Kenya

      A Guide from an Advocate Perspective https://muteamuthuriadvocates.com/blog/turnover-tax-kenya A Complete Guide Directly from KRA https://www.kra.go.ke/helping-tax-payers/faqs/introduction-to-itax

SMEs Hapa Kenya Tunapenda Cash Sana… But At What Cost?

  Wasee wengi wana-run biashara huku Kenya wanaamini kitu moja bila kuquestion: “Kulipa cash ndio safest. Cash ndio inaweka biashara safe.” Na juu tumezoea culture ya kuavoid madeni, tunafeel kama kulipa kitu full immediately ni sign ya discipline.  Lakini what if hiyo belief ndio inafanya biashara yako ikuwe slower kuliko venye inafaa? Imagine una stock opportunity imejitokeza, ama unataka kuongeza marketing budget juu demand imeanza kupanda… lakini cash yote imeshikiliwa mahali moja juu ulilipa kila kitu upfront.  Suddenly unakosa flexibility. Na biashara bila flexibility, mara mingi hukua vulnerable kuliko venye owner anarealize. The uncomfortable truth ni hii: cash inaweza kua quietly draining your business growth. Big companies hawakai na pesa yao yote locked kwa one place. Wanajua leverage. Wanajua kutumia financing options, installment models, na systems zenye zinaacha cash flow yao ikiwa free for expansion, marketing, na grabbing opportunities faster kuliko com...